Friday, November 14, 2008

Ndege zilitumika kufanyia Ughaidi huu



Ndege zilitumika kufanyia Ughaidi huu
.1. American Airlines Flight 11, iliyotumiwa kugonga mnara wa Kaskazini mwa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) la mjini New York mnamo saa 8:46:30 asubuhi.
2. United Airlines Flight 175, ilitumiwa kugonga mnara wa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) la Kusini mnamo saa 9:02:59 asubuhi. Watu wengi waliona tukio la pili kwasababu habari zilikuwa tayari zishasambaa katika mji na kila kamera za televisheni zilikuwa zikielekezea macho yao huko katika eneo la tukio, na wakati huo huo ndege ya pili ikagonga tena mnara wa Kusini mwa Jengo hilo.
3. American Airlines Flight 77, ilitumiwa kugonga jengo la Pentagon la mjini Arlington, Virginia (karibu kidogo na Washington DC), mnamo saa 9:37:46 asubuhi.
4. United Airlines Flight 93, hii haikubahatika kugonga mahala popote pale, badala yake wakaiangusha chini mnamo saa 10:03:11 asubuhi. Yaaminika ya kwamba magaidi hao walikuwa wakitaka kuigonga ndege hiyo katika jengo la mji mkuu wa Marekani. Abiria walijaribu kuinyang'anya Ndege hiyo kutoka mikononi mwa magaidi hao lakini hawakufanikiwa. Na matokeo Ndege ikashia kuanguka karibu na mji wa Shanksville, Pennsylvania.

No comments: